Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399
Na Vijimambo
Mhubiri wa kimataifa na mchekeshaji maarufu Emmanuel Mgaya au jina
maarufu Masanja Mkandamizaji juzi alitembelea studio za kuzalisha muziki
na video za SamSPRO Studios zilizoko Washington, DC.
Masanja kama anavyoonekana kwenye picha aliambatana na waimbaji wa
nyimbo za injili Milca Kakete kutoka Canada na Milca Thomas kutoka North
Carolina, pamoja na baadhi ya waimbaji wa kundi la The Sound of Glory
kutoka kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries lililoko
Washington DC ambako mwigizaji huyo maarufu alikuwepo kama mhubiri mkuu
wa mkutano uliokuwa ukiendelea kwa siku tatu mfululizo.
Akijibu swali alipoulizwa juu ya ugeni huo studioni hapo producer na
mmiliki wa studio hiyo ndugu Samuel Malonja alisema kuwa Masanja aliamua
kutafuta studio ambayo anaweza kuitumia kurekodi wimbo wake, hilo ndio
lilikuwa lengo la ugeni huo.
Masanja amerekodi wimbo mmoja katika studio hiyo akiwashirikisha
waimbaji wengine wa injili akiwemo Milca Kakete kutoka Canada, Milca
Thomas kutoka North Carolina na waimbaji wa kanisa la The Way of the
Cross Gospel Ministries la mjini Washington DC.
Picha hapo chini zinaonyesha kazi ya kurekodi wimbo huo chini ya
producer Sam ikiendelea huku Masanja akionekana kusimamia zoezi hilo kwa
umakini kabisa.
No comments:
Post a Comment