Social Icons

Pages

Featured Posts

Tuesday, January 19, 2016

MATUMAINI NA UJIO WAHAMA KAOLE WALAMBA SHAVU TBC1

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 
Matumaini na Ujio wakikamua katika moja ya Scene
 Wakiwa pamoja na Muongozaji wa kipindi hicho Johackim Kapembe kutoka TBC 1
 Wakiwa pamoja na muongozaji msaidizi wa Kipindi 
Wasanii wa Komedi Bongo zao la Kaole Sanaa Group, Ujio na Matumaini, wamepata shavu la kurusha maigizo yao kupitia televisheni ya Taifa ‘TBC 1’ hiyo ikiwa ni moja ya malengo ya wasanii hao kufanya kazi zenye tija kwa mwaka huu.

Wakipiga stori na paparazzi wetu, Ujio na Matumaini walisema kuwa huu ni muda sahihi wa wao kujitegemea zaidi na kuwashukuru wasanii wenzao waliofanya nao kazi kwa karibu enzi za Kaole kuanzia Ray Kigosi, Marehemu Kanumba, Kipemba, Chiki Mchoma, Cheni, Tito, Branko , Kissa na wengine wengi. 

Naye muandaaji wa kipindi hicho, Johakim Kapembe wa TBC alisema kuwa ameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa wanavipaji vikubwa vya komedi na mashabiki wengi.


HAWA JAMAA NI KAMA DIZAINI FLANI WANAMUIGA SHARO MILIONEA, NANI MKALI ZAIDI? CHEKI HAPA

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 
 Mtu Chuma Aka Sharo Machozi katika Ubora wake
 Stan Bakora nae katika Ubora wake

Tuandikie maoni yako

 

Wednesday, August 19, 2015

HOT: KINGWENDU ACHUKUA FOMU YA UBUNGE

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399
Kingwendu akikabidhiwa fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kisalawe kwa tiketi ya CUF.
Katika hali ya kuonyesha kuwa UKAWA imedhamiria kushika dola, mgombea wa ubunge jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya Chama Cha wananchi (CUF),  Rashid Mwinshehe 'Kingwendu' jana amechukua fomu ya ubunge na kuahidi kuwa muda wa kwenda kubutua mijicho yake na kutoa ulimi nje umewadia, huu ndio muda wa heno heno.

Tuesday, August 18, 2015

MASANJA MKANDAMIZAJI ATEMBELEA SamSPRO Studio WASHINGTON, DC

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

Na Vijimambo


Mhubiri wa kimataifa na mchekeshaji maarufu Emmanuel Mgaya au jina maarufu Masanja Mkandamizaji juzi alitembelea studio za kuzalisha muziki na video za SamSPRO Studios zilizoko Washington, DC. Masanja kama anavyoonekana kwenye picha aliambatana na waimbaji wa nyimbo za injili Milca Kakete kutoka Canada na Milca Thomas kutoka North Carolina, pamoja na baadhi ya waimbaji wa kundi la The Sound of Glory kutoka kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries lililoko Washington DC ambako mwigizaji huyo maarufu alikuwepo kama mhubiri mkuu wa mkutano uliokuwa ukiendelea kwa siku tatu mfululizo. Akijibu swali alipoulizwa juu ya ugeni huo studioni hapo producer na mmiliki wa studio hiyo ndugu Samuel Malonja alisema kuwa Masanja aliamua kutafuta studio ambayo anaweza kuitumia kurekodi wimbo wake, hilo ndio lilikuwa lengo la ugeni huo. Masanja amerekodi wimbo mmoja katika studio hiyo akiwashirikisha waimbaji wengine wa injili akiwemo Milca Kakete kutoka Canada, Milca Thomas kutoka North Carolina na waimbaji wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries la mjini Washington DC. Picha hapo chini zinaonyesha kazi ya kurekodi wimbo huo chini ya producer Sam ikiendelea huku Masanja akionekana kusimamia zoezi hilo kwa umakini kabisa.

Wednesday, June 10, 2015

BREAKING NUUUUZ .. HOOOOOT: PICHA... MCHEKESHAJI MAARUFU MKWERE APATA TOTO LA KIKE .. AMUONESHA LIVE HAPA....

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

 Huyu ndiye Mtoto wa Mchekeshaji Mkwere,Nurat ambaye unamuona kwa Mara ya kwanza kabisa hapa
 Mkwere akifurahi na Mtoto wake
 Baba mama na Mtoto

Picha na Komedi Zone

Friday, June 5, 2015

Wasanii wa komedi wakesha wakijifua kwa ajili ya muvi yao mpya

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 
 Direkta wa muvi hiyo, Sarah Albert Nduma akiwaelekeza wasanii jambo kwenye script.
 Wasanii wakijadiliana uhusika wao.
Etii
 Msanii, Ujio na Mkono Mkonole wakijaribu kuigiza baada ya vipande vya muvi hiyo.
 Mazoezi yakiendelea.
 Picha na Komedi Zone
Kamera ya Komedi Zone wiki hii imewamulika wasanii wa komedi wakifanya mazoezi kwa ajili ya muvi yao mpya ambayo kwa mujibu wa mwenyekiti wao, Sumaku, inatajwa kama muvi ya mapinduzi mapya ya komedi Bongo.

Kamera yetu iliwanasa wasanii hao wakiwa wamepiga kambi katika Hoteli ya Ndekha ambapo ndiyo makao makuu yao maeneo ya Magomeni Mwembechai jijini Dar wakifanya mazoezi bila kuchoka usiku mzima huku wakitarajia kuendelea kwa muda wa wiki nzima ya mazoezi kabla ya kuingia kwenye zoezi la kupiga picha.

ETI STAN BAKORA ANASEMA HIVI: STAILI ZA NYWELE ZANGU NI KUMBUKUMBU YA SHARO MILIONEA

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 


Msanii wa komedi bongo anayepanda kwa kasi kwenye tasnia hiyo, Stan Bakora amefungukia staili yake ya nywele kuwa ni kumbukumbu tosha kwake ya kumuenzi marehemu Sharo Milionea aliyekuwa mkali wa vichekesho na Bongo Fleva.

Akipiga stori na Komedi zone, Stan Bakora alisema kuwa alikutana na marehemu Sharo miezi michache kabla hajafariki akiwa Morogoro ambapo aligundua kipaji chake cha kuchekesha na kumtambulisha kwa Kitale ili wafanye kazi pamoja.

“Jamaa alinikubali sana akanitambulisha kwa Kitale na kumwambia kuwa tutakuwa tukifanya kazi wote, sikujua kumbe ndiyo miezi kadhaa anakuja kupata ajali mbaya na kufariki tukiwa hatujafanya kazi hata moja,” alisema Stan Bakora.

Stan Bakora aliongeza kuwa baada ya msiba huo ndipo Kitale alimtafuta ili kutimiza maneno ya marehemu Sharo kwamba wafanye kazi pamoja.

“Kweli tunafanya kazi pamoja na braza Kitale, namkubali sana Sharo Milionea tangu awali na kuonesha kuwa jamaa alikuwa mtu muhimu kwangu ndiyo maana nimeamua kuweka staili ya nywele kama yeye japo kuwa uigizaji wangu ni tofauti kabisa na wake, alisema Stan Bakora.

Na Komedi zone
 

HOT HOT: MSANII MWENYE MBWEMBWE NYINGI NISHA AWACHANA WANAODAI YEYE ANAPENDA WANAUME WENYE PESA MOB.

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 

Msanii wa Komedi Bongo anayetamba na muvi yake ya Mtaa kwa Mtaa, Salma Jabu maarufu kwa jina la Nisha amewafungukia watu wanaodai kuwa yeye anapenda wanaume wenye pesa na kudai kuwa haangalii kigezo hicho bali ni mapenzi ya kweli kutoka kwa mtu.

Nisha alifunguka hayo kwenye mahojiano katika kipindi cha filamu kinachorushwa na Channel 10, ambapo pamoja na hayo aliizungumzia muvi yake ya Mtaa kwa Mtaa, na kusema kuwa moja kati ya scene zilizomfurahisha ni pamoja na ile waliyovaa kama askari na kusimamisha magari barabarani ambapo wengi wa madereva waliokuwa wakitumia barabara hiyo walisimama kweli wakiwadhania ni matrafiki kweli.

“Yaani kuna wengine walikuwa wakitetemeka kabisa walipotuona waliamini kuwa sisi ni askari kabisa,” alisema Nisha.

Na Komedi zone

MWIGIZAJI MKONGWE TANZANIA, MZEE JANGALA KUTANGAZA NIA

Mwigizaji mkongwe nchini Bakari Malembela maarufu kama Mzee Jangala.

Dar es Salaam.
Mwigizaji mkongwe nchini, Bakari Mbelemba, maarufu kwa jina la kisanii la Mzee Jangala, amesema atatumia Tamasha la Ngoma za Asili “kutangaza nia ya kugombea urais” wa Jamhuri ya Muungano.


Tamasha hilo litafanyika Juni 13 kwenye Uwanja wa Taifa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal amealikwa kuwa mgeni rasmi.


Akizungumza na gazeti hili kwenye ofisi za gazeti la Mwananchi jana, Mzee Jangala alisema ana haki na sifa zote za kugombea nafasi hiyo ya juu, kama waliotangulia kutangaza nia na kuwataka wananchi kutombeza kwa uamuzi wake.


Mzee Jangala, ambaye mara nyingi huigiza kama mzee mbishi na mwenye kauli za vichekesho, amesema Watanzania hawana budi kusubiri kusikia sera zake na mikakati yake endapo akifanikiwa kupata nafasi hiyo.


“Nimepanga kutangaza nia ya kugombea urais siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa mbele ya Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal, ambaye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la kihistoria la ngoma za asili,” alisema Mzee Jangala.


“Najua watu watafikiria natania katika jambo hili. Lakini siko hivyo. Nina uhakika na ninachokisema kwani ni haki ya kila raia na inatambulika kikatiba kugombea nafasi hii nyeti endapo tu ukiwa unazo sifa na vigezo,” alisema Mzee Jangala.


Msanii huyo mkongwe, ambaye hakutaja atagombea kwa chama gani, alisema kilichomsukuma kutangaza nia kwanza ni mzalendo na mapenzi kwa nchi yake.


“Pili ni kuondoa tatizo la mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana na wananchi,” alisema msanii huyo aliyeanzia katika uigizaji wa jukwaani.


Alisema baadhi ya viongozi wakipewa madaraka wanasahau walikotoka na kutenda mambo kinyume na matarajio ya wananchi. Hali inayosababisha shughuli wanazozifanya kutofanyika ipasavyo na kuibua minung’uniko.


“Hawa tuliowachagua, baadhi yao hawana uchungu na nchi hii ndiyo maana rushwa imekuwa sehemu ya maisha yetu, kwa sababu walioko madarakani wapo kwa masilahi yao binafsi na si ya Watanzania,” alisema Mzee Jangala.


“Rushwa imekuwa changamoto mojawapo, sasa basi mimi nina uwezo, najiamini kuongoza na kupambana na jambo hili. Kinachohitajika kwa Watanzania kuniunga mkono pindi nitakapotangaza nia yangu.”


Hata hivyo, Mzee Jangala hakuwa tayari kutaja vipaumbele vyake endapo atapata nafasi ya kugombea urais akisema kuwa bado ni mapema sana. Ukizingatia kuna wimbi kubwa la Watanzania wanaotarajia kutangaza nia ya nafasi hiyo.


Pia, aliwataka wananchi kuachana na fikra kuwa mwaka huu nchi hii kiongozi anatakiwa kuwa kijana hata wazee wana uwezo, kinachohitajika ni sifa na hekima.


“Urais hauna kijana wala mzee kinachohitajika ni je? Una sifa na uzalendo kutoka moyoni. Sitaki ubunge nia yangu ni kuwasaidia Watanzania endapo nikapata ridhaa ya kuongoza nchi kupitia nafasi ya urais,” alisema Mzee Jangala ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mafanikio ya Muda Mrefu Katika Fani.


alifanikiwa kunyakuwa tuzo ya maisha kutokana na mchango wake mkubwa katika sanaa ya filamu na vichekesho, kutokana na uchapakazi na hekima aliyonayo.MWANANCHI 

 Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

Tuesday, June 2, 2015

HII KALI: ULOKOLE WAMUHENYESHA MATUMAINI NI BAADA YA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU KUIGIZA KAMA MLEVI.

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 

Matumaini wa sasa....
 
Msanii anayerudi kwa kasi katika tasnia ya komedi Bongo, Matumaini, amefunguka jinsi alivyopata tabu kuigiza kama mke mlevi katika muvi yao mpya ambayo ipo sokoni ya Shida, Vumilia na Tabu inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Akizungumza na Komedi Zone, Matumaini alisema kuwa alihangaika sana kuigiza kama mke mlevi kutokana na imani yake ya sasa ya kilokole ambapo alisema kwa kuwa yeye ni msanii na lengo ni kuelimisha jamii alijitahidi na kufanya muvi hiyo kwa kiwango kilichotakiwa,
"Ilikuwa ngumu sana lakini huwezi amini nilikamua sana kipande changu na mwishoni kazi ilikuwa nzuri sana," alisema Matumaini.

Na Komedi zone