Social Icons

Pages

Tuesday, January 19, 2016

MATUMAINI NA UJIO WAHAMA KAOLE WALAMBA SHAVU TBC1

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 
Matumaini na Ujio wakikamua katika moja ya Scene
 Wakiwa pamoja na Muongozaji wa kipindi hicho Johackim Kapembe kutoka TBC 1
 Wakiwa pamoja na muongozaji msaidizi wa Kipindi 
Wasanii wa Komedi Bongo zao la Kaole Sanaa Group, Ujio na Matumaini, wamepata shavu la kurusha maigizo yao kupitia televisheni ya Taifa ‘TBC 1’ hiyo ikiwa ni moja ya malengo ya wasanii hao kufanya kazi zenye tija kwa mwaka huu.

Wakipiga stori na paparazzi wetu, Ujio na Matumaini walisema kuwa huu ni muda sahihi wa wao kujitegemea zaidi na kuwashukuru wasanii wenzao waliofanya nao kazi kwa karibu enzi za Kaole kuanzia Ray Kigosi, Marehemu Kanumba, Kipemba, Chiki Mchoma, Cheni, Tito, Branko , Kissa na wengine wengi. 

Naye muandaaji wa kipindi hicho, Johakim Kapembe wa TBC alisema kuwa ameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa wanavipaji vikubwa vya komedi na mashabiki wengi.


No comments:

Post a Comment