Social Icons

Pages

Friday, June 5, 2015

HOT HOT: MSANII MWENYE MBWEMBWE NYINGI NISHA AWACHANA WANAODAI YEYE ANAPENDA WANAUME WENYE PESA MOB.

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 

Msanii wa Komedi Bongo anayetamba na muvi yake ya Mtaa kwa Mtaa, Salma Jabu maarufu kwa jina la Nisha amewafungukia watu wanaodai kuwa yeye anapenda wanaume wenye pesa na kudai kuwa haangalii kigezo hicho bali ni mapenzi ya kweli kutoka kwa mtu.

Nisha alifunguka hayo kwenye mahojiano katika kipindi cha filamu kinachorushwa na Channel 10, ambapo pamoja na hayo aliizungumzia muvi yake ya Mtaa kwa Mtaa, na kusema kuwa moja kati ya scene zilizomfurahisha ni pamoja na ile waliyovaa kama askari na kusimamisha magari barabarani ambapo wengi wa madereva waliokuwa wakitumia barabara hiyo walisimama kweli wakiwadhania ni matrafiki kweli.

“Yaani kuna wengine walikuwa wakitetemeka kabisa walipotuona waliamini kuwa sisi ni askari kabisa,” alisema Nisha.

Na Komedi zone

No comments:

Post a Comment