Social Icons

Pages

Friday, June 5, 2015

ETI STAN BAKORA ANASEMA HIVI: STAILI ZA NYWELE ZANGU NI KUMBUKUMBU YA SHARO MILIONEA

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 


Msanii wa komedi bongo anayepanda kwa kasi kwenye tasnia hiyo, Stan Bakora amefungukia staili yake ya nywele kuwa ni kumbukumbu tosha kwake ya kumuenzi marehemu Sharo Milionea aliyekuwa mkali wa vichekesho na Bongo Fleva.

Akipiga stori na Komedi zone, Stan Bakora alisema kuwa alikutana na marehemu Sharo miezi michache kabla hajafariki akiwa Morogoro ambapo aligundua kipaji chake cha kuchekesha na kumtambulisha kwa Kitale ili wafanye kazi pamoja.

“Jamaa alinikubali sana akanitambulisha kwa Kitale na kumwambia kuwa tutakuwa tukifanya kazi wote, sikujua kumbe ndiyo miezi kadhaa anakuja kupata ajali mbaya na kufariki tukiwa hatujafanya kazi hata moja,” alisema Stan Bakora.

Stan Bakora aliongeza kuwa baada ya msiba huo ndipo Kitale alimtafuta ili kutimiza maneno ya marehemu Sharo kwamba wafanye kazi pamoja.

“Kweli tunafanya kazi pamoja na braza Kitale, namkubali sana Sharo Milionea tangu awali na kuonesha kuwa jamaa alikuwa mtu muhimu kwangu ndiyo maana nimeamua kuweka staili ya nywele kama yeye japo kuwa uigizaji wangu ni tofauti kabisa na wake, alisema Stan Bakora.

Na Komedi zone
 

No comments:

Post a Comment