
 Matumaini na Kiwewe wakiwa katika ubora wao
Msanii wa Komedi Bongo, Kiwewe amefungukia uhusiano wake wa sasa na msanii mwenzake wa kike aliyewahi kutamba naye enzi hizo, Matumani akidai kuwa bado ni marafiki tofauti na watu wanavyofikiri.
Akizungumza na mwandishi wetu wa Komedi Zone, Kiwewe alisema kuwa watu wengi wanadhani amegombana na Matumaini ndiyo maana hawafanyi kazi pamoja siku hizi jambo ambalo siyo kweli na kuongeza kuwa kazi na mikataba tofauti, ndiyo kitu kinachowafanya wasiwe pamoja kikazi kama zamani.
"Matumaini ni best yangu mkubwa, mashabiki wangu wafahamu tu kuwa tunatenganishwa na kazi mbalimbali, yeye ana kazi zake na mimi nina kazi zangu lakini huwa tunakutana mara kwa mara," alisema Matumaini.
Na Komedi zone
Na Komedi zone
No comments:
Post a Comment