Social Icons

Pages

Friday, May 15, 2015

ZIMWI AFUNGUKA: KUNA WASANII FREEMASONS

Zimwi akiwa katika Poziii....

Msanii wa komedi anayejulikana kwa sauti yake na uwezo wa kunyumbua sura huku akivunja mbavu za watu, Zimwi, amesema kuwa anaamini kuna wasanii Freemason katika tasnia mbalimbali Bongo.

Akizungumza na Komedi Zone, Zimwi alisema kuwa pamoja na watu wengi kutoamini ushirikina na imani za kifreemason, yeye binafsi anaamini kuna watu hao miongoni mwa wasanii na kusema kuwa baadhi yao ni wale wanaoonekana kufanikiwa kimaajabu kuliko kazi wanazozifanya huku wanaojituma wakiendelea kuwa masikini na kutofanikiwa kabisa.
"Wapo wasanii wa aina hiyo maana unakuta hawafanyi kazi wala nini, lakini wanafanikiwa na wale wanaofanya kazi kwa jasho lao  ndio hawatoki kabisa," alisema Zimwi.

No comments:

Post a Comment