Msanii wa komedi anayetamba na brandi yake ya Mkude Simba, Kitale, amevunja ukimya na kudai kuwa hajafulia kama watu wanavyodhania.
Akizungumza na Komedi Zone, Kitale alisema kuwa amekuwa kimya kwa sababu anajipanga upya kwa ajili ya ujio wa pili ambao mwenyewe amedai ni zaidi ya Mkude Simba.
"Nimeshuka kidogo lakini siyo kiviile! na hii yote ni kutokana na kujipanga zaidi maana kuna bonge la project ambalo ni zaidi ya Mkude Simba linakuja soon," alisema Kitale.

No comments:
Post a Comment