Msanii wa filamu mseto yaani za visa vya kuchekesha na serious, Kulwa Kikumba 'Dude' amesimulia alivyosahau na kujikuta akiitafuta suruali aliyoivaa kwa masaa mawili bila kujua.
 Akizungumza na Komedi Zone, Dude alisema kuwa siku ya tukio alikuwa lokesheni ambapo baada ya kushuti muvi alivaa suruali yake hiyo bila kujua na kuanza kuitafuta kwa muda mrefu hadi akaamua kwenda kwa wasanii wenzake kuwauliza kama wameiona.
 "Wenzangu wakajiunga na mimi tukaanza kuitafuta sasa baadaye mmoja wetu akaniuliza suruali ya khaki unayoitafuta si hiyo uliyoivaa..nikaiangalia kumbe kweli," alisema Dude.

No comments:
Post a Comment