Social Icons

Pages

Monday, May 25, 2015

MATUMAINI SHAVU DODO

Matumaini hivi sasa 
 Kipindi anaumwa


Staa wa Komedi Bongo aliyewahi kuwika kipindi cha nyuma akiigiza na staa mwenziye wa kiume, Kiwewe, Matumaini, amewashangaza mashabiki zake kwa kuwa 'shavu dodo' kwa sasa huku akionekana kuridhika tofauti na alivyokuwa miezi michache nyuma.

Kwa mujibu wa udadavuzi, Komedi Zone ilizinyaka picha za staa huyo zikiwa kwenye profile yake ya mtandao wa Whatsapp ambapo wengi wa mashabiki wake walioziona walimsifia kwa kuonekana amenenepa huku wengine wakishangaa.

Tujikumbushe, Matumaini aliwahi kupata misukosuko ya hapa na pale iliyotokana na kuugua ghafla akiwa nchini Msumbiji, aliporudi nchini kwa ajili ya matibabu alitangaza kuokoka na hatimaye kutulia kuigiza hadi sasa. 

Na Komedi zone

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

No comments:

Post a Comment