Social Icons

Pages

Monday, May 25, 2015

SUMAKU: KOMEDI IPO KATIKA MABADILIKO MAKUBWA


Mkurugenzi  wa chama cha wasanii wa komedi Tanzania (Tanzakomedi) Sumaku amesema kuwa kwa sasa chama cha komedi kipo katika mabadiliko mbalimbali ili kuboresha maslahi ya wasanii wa fani hiyo nchini.

Akizungumza na Komedi Zone, Mkurugenzi huyo alikiri kuwepo kwa changamoto mbalimbali za wanakomedi hali inayowashushia thamani japo kuwa kazi zao zinapendwa na kukubalika na watu mbalimbali katika jamii.

"Kwa sasa tupo katika mabadiliko makubwa ya kimtazamo na ufanyaji wetu wa kazi ili kuirudisha thamani yetu ambayo ndiyo hasa tumeikosa, mikakati ni mingi na zaidi tumejipanga na kujijenga mwaka huu ili kila kitu kiwe vizuri," alisema Sumaku. 
Na komedi zone

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

No comments:

Post a Comment