Social Icons

Pages

Friday, May 22, 2015

HOT NEWS: UKWA WA BONGO MOVIE ATOSWA WAIFU KISA USANII


Msanii wa Komedi, Morgan Ngoda maarufu kama ‘Ukwa wa Bongo’, amesimulia jinsi kazi yake ya kuigiza ilivyovunja penzi lake na mchumba wake wa siku nyingi aliyepanga kumuoa.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Ukwa alisema kuwa akiwa katika michakato ya kutambulishana kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uchumba, wazazi wa mpenzi wake walitaka kujua kazi yake ndipo alipowaambia kuwa ni msanii wa Bongo Muvi, jambo lililowachefua wakwe hao waliodai Bongo Muvi imejaa ufuska na hafai kumuoa msichana huyo.
“Yaani wale wazazi hawakukubali kabisa utetezi wangu walinidai moja kwa moja kuwa mimi ni kama wenzangu wa Bongo Muvi, wakanitaka nikae mbali na mtoto wao, na kweli kuanzi siku hiyo mimi na mipango ya kuoa basi tena,” alisema Ukwa.

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

No comments:

Post a Comment