Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399
 Mwigizaji
 wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),akipewa maelekezo 
ya kuendesha Trekta mara Baada kukabidhiwa ufunguo wake na  Fundi
 Mkuu wa Kampuni ya Farm Equip Tanzania , Yunusu Nsekela wakati wa 
kukabidhiwa Matrekta kwaajili ya kilimo jijini Dar es Salaam leo
 Mwakilishi
 wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta 
lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
 Mwakilishi
 wa muigizaji Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta 
lake kwa sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink  akisalimiana
 mara baada ya akimkabidhi ufungua wa Trekta lake Mwigizaji wa Origino 
Komed, Isaya Mwakilasa(Wakuvanga) jijini Dar es Salaam leo.
  Mwigizaji
 wa Origino Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee) akishukuru kwa 
niaba ya waigizaji wa kundi la Origino Komedi  mara baada ya kukabidhiwa
 Funguo za Matrekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto 
ni Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif 
Sheink,Isaya Mwakilasa(Wakuvanga ),Lucacy Mhavile(Joti) na kulia ni Alex Chalamila(Mackregani).
  Mkurugenzi
 Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akizungumza
 na Vijana wa Kundi la Origino    Komedi mara baada ya kuwakabidhi 
funguo za Matrekta ya kilimo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink , katika picha ya pamoja waigizaji wa kundi la Origino  Komedi na nyuma yao ni Matrekta ambayo wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano ya Matrekta ya Kilimo kati ya Mkurugenzi
 Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink na 
Waigizaji wa kundi la Origino Komedi, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
 ya Matrekta ya Kilimo ambayo waigizaji wa Kundi la Original Comedi 
wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya 
Jamii.
Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
WAIGIZAJI
 wa kindi cha Origino Komedi  wamewaasa vijana kutumia vipaji vyao ili 
kutengeneza maisha yao kuwa  mazuri na sio kufikiri kuwa vijana wengi 
hushikwa mkono na mtu ili kufanikiwa.
Hayo
 yamesemwa na kundi la waigizaji wa Origino Komedi wakati wa kukabidhiwa
 Matrekta ya Kilimo aina ya Sonalika kutoka kampuni ya Farm Equip 
Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
 Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink amesema 
kuwa  vijana  wameamua kufanya jambo la maana kwa jamii ,"kwani 
wamenunua matrekta kwa ajili ya kilimo,vijana wengi wamekuwa wakinunua 
magari ya kifahari  bila kujua kunakesho na keshokutwa kwa maendeleo 
yao",alisema Bwa Arif.
Nae
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewapongeza vijana wa kundi 
hilo kuwa kufanya maamuzi sahihi na ya maendeleo kwa kununua Matrekta 
hayo kwaajili ya kilimo,amesema kuwa uamuzi wao ni mzuri hata kwa jamii 
kwani pia kwa namna moja ama nyingine itasaidia kuongeza ajira kwa 
vijana,kwakuwa kilimo kinahitaji watu wengine na sio wao wenyewe watakao
 weza kuendesha Matrekta hayo mashambani.
Kundi
 hilo la Origino Komedi  linaundwa na vijana 7 ambao ni Alex 
Chalamila(Mackregani),Josef Shamba(Vengu),Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani 
Mzee),Lucacy Mhavile(Joti), Isaya Mwakilasa(Wakuvanga),Emmanuel 
Mgaya(Masanja mkandamizaji) na Davidi Seki.
 Waigizaji hao wameahidi kupoleka Matrekta yao kwenda kubeba takataka katika Wilaya
 ya Kinondoni ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda atazindua
  kampeni ya Ona aibu, ambayo itahamasisha usafi katika Wilaya ya 
Kinondoni.
No comments:
Post a Comment