Social Icons

Pages

Friday, May 29, 2015

AKI WA BONGO MUVI ASIMULIA UTAMU WA NDOA YAKE



Msanii wa Komedi Bongo, Meya Shabani maarufu kama 'Aki wa Bongo Muvi', amesimulia raha ya ndoa yake aliyofunga mwaka jana na aliyekuwa mchumba wake, Amina Shabani na kusema kuwa si kama wengi wanavyodai kuwa ndoa ni karaha.

Akipiga stori na Komedi Zone baada ya kutembelewa ofisini kwake maeneo ya Mwananyamala Kisiwani jijini Dar, Aki alisema kuwa watu wengi wanadhani ukioa ndiyo gharama ya maisha inapanda na kutingwa na mambo mengi jambo ambalo amelikataa na kudai kuwa ndoa ina mambo mengi mazuri.

"Si unaniona hata shavu limeanza kunitoka kama ningekuwa nina shida nisingekuwa hivi," alisema Aki na kuongeza kuwa kwa sasa ndoa yake anatarajia kupata mtoto kwa kuwa mkewe ana mimba ya miezi sita.
Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399.


No comments:

Post a Comment