Social Icons

Pages

Friday, May 29, 2015

MSANII WA KOMEDI ASHA BOKO AWATAKA WASANII WENZAKE WAUNGANE , AWAPONGEZA ORIGINO KOMEDI


Wakiwa Location

Mwanamama mwenye umbo la kibabe, ndani ya tasnia ya vichekesho, Asha Boko amewaasa wasanii wenzake wa Komedi Tanzania kutokata tamaa katika harakati zao za kutoka kisanii sambamba na kuwapongeza Orijino Komedi kwa kulamba mshiko mnene.
Akipiga stori na Komedi Zone, Asha Boko alisema kuwa sanaa ya komedi au uchekeshaji inapendwa sana duniani hivyo inalipa vizuri na kuongeza kuwa wasanii wa komedi nchini wanapaswa kuungana na kufanya vitu kwa umoja ili kusonga mbele kimafanikio.
Mbali na ushauri huo Asha Boko aliwapongeza wasanii nguli wa Orijino Komedi kwa kuendelea kuiwakilisha tasnia ya komedi vyema na kuonesha mfano mzuri wa kuigwa na wasanii wengine.
"Lazima tufanye kazi zetu ziwe nzuri na tuwe na umoja kupitia chama chetu ili tusonge mbele kisanaa na kuboresha kipato chetu, cha msingi tusikate tamaa tukiamua tutafika popote. Nawapongeza sana wenzetu wa Orijino Komedi walivyoonesha mfano," alisema Asha Boko.
Tujikumbushe; Orijino Komedi, jana walipokea zawadi ya matrekta yenye thamani ya sh. mil 120 kutoka kwa kampuni ya Farm Equip ltd, hiyo ikiwa ni miezi michache baada ya kukabidhiwa nyumba na shirika la Nssf na baadaye bima ya afya.

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

No comments:

Post a Comment