Social Icons

Pages

Monday, June 1, 2015

HOT NEWS: MKWERE ASIMULIA MKASA WA WALIOTAKA KUMFUMANIA JINSI WALIVYOUMBUKA.

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 

Msanii wa komedi anayeuza sura kupitia kipindi cha Mizengwe kinachorushwa kupitia chaneli ya ITV, Hemedi Maliyaga maarufu "Mkwere", amewataka mashabiki wake kutomchukulia vibaya kutokana na kushinda sana hotelini. 

Akizungumza na Komedi Zone, Mkwere alisema kuwa analazimika kuingia kwenye hoteli moja inayotajwa kwa jina la Ndekha iliyopo Magomeni Mwembe Chai kwa kuwa ni makao makuu ya chama cha komedi Tanzania (TANZACOMEDY) pia ni makao makuu ya Kashikashi Entertainment ambapo yeye ni mmoja kati ya wasanii hao. 

Mbali na hayo Mkwere alisimulia ambavyo kundi fulani la watu walivyofika hotelini hapo kwa lengo la kumfumania walivyoumbuka baada ya kumkuta akiwa ofisini kwake (ndani ya hoteli hiyo) akichapa kazi. 

"Kuna kipindi watu fulani walikuja mpaka hapa wakataka kunifumania walidhani nimekuja na mchepuko. Inaonekana walinifuatilia nikiwa mpaka napaki gari hapo nje. Sasa niliposhuka na kuingia hotelini wakadhani ndiyo nakuja kumaliza. Wakaumbuka waliposikia hapa ni ofisini kwetu na kweli wakanikuta nachapa kazi;" alisema Mkwere. 

No comments:

Post a Comment