Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399

Huu ndio msosi na mahanjamu
Msanii wa komedi, Nicholaus Ngoda a.k.a Ukwa wa Bongo Muvi
amejikuta akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa majonzi baada ya afya ya mama
yake mzazi kudorora hali iliyomlazimu akatishe mipango ya kuangusha pati kwa
ajili ya siku hiyo kama alivyopania.
Kamera ya Komedi Zone ilimnasa msanii huyo Juni 1 mwaka huu nyumbani kwa mama
yake maeneo ya Kiwalani Bombomu jijini Dar alipoenda kumtembelea ambapo msanii
huyo alimua kusherehekea siku hiyo kwa kumuangushia msosi wa ‘kinyumbaninyumbani’
mama yake mzazi aliyemtambulisha kwa jina la Agnes George.
“Dah kaka siku yangu ya kuzaliwa ilijaa huzuni kidogo mama
yangu anaumwa hivyo nilienda kumtembelea na nikafanyia sherehe kwake,tena
sikutaka keki wala nini tulikula ugali wa mhogo, samaki wakukaanga, kachumbali
na bamia za kuunga, in short nilifurahia sana kusherehekea na mama yangu,”
alisema Ukwa.
NA KOMEDI ZONE
No comments:
Post a Comment