Nisha akiwa katika sare za polisi katika muvi yake ya Mtaa kwa Mtaa inayotarajiwa kutoka hivi karibuni
Picha ya gari la Nisha lililovunjwa na kuibwa fedha
Msanii
mrembo kunako maigizo ya komedi,Nisha Jabu ameshukuru Mungu baada ya
kunusurika kuuawa na majambazi waliovamia nyumbani kwake mapema wiki
iliyopita na kumuibia mamilioni ya fedha.
Nisha
alisema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo katika post yake
alimshukuru Mungu kwa kumnusuru na kuita jambo hilo kama majaribu huku
pia akiwashukuru watu mbalimbali waliompa pole.
"Hata Nabii Ayubu alipata majaribu kama haya. Namshukuru Mungu sikudhurika pia nawashukuru wote mlionipa pole,"alisema Nisha.


No comments:
Post a Comment