Social Icons

Pages

Tuesday, May 19, 2015

CHAKUSAHAU! FUNGUO NUSURA IMLAZE DUDE NJE


Msanii wa maigizo Bongo, Dude almanusura alale nje baada ya kusahau alipoweka funguo za gari yake aina Toyota Mark II na kuzitafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.

Tukio hilo lilitokea juzi kati wakiwa lokesheni mitaa ya Mbezi Beach jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa amemaliza kushuti filamu ambapo alikuwa amejiandaa kuondoka na kushangaa akiwa hana funguo ya gari.

Kwa mujibu wa mashuhuda walidai kuwa jamaa alihangaika sana kiasi kwamba alikuwa akirudiarudia kujisachi mifukoni mwake lakini cha kushangaza alipokata tamaa aliiona funguo yake ikiwa inaning'inia kwenye mlango wa gari lake jambo lililoonesha kuwa hakuwa ameichomoa aliposhuka kwenye gari.

Komedi Zone ilipomtafuta Dude alisema kuwa alikosa raha kiasi cha kumfanya asitamani kulala nyumbani Kwa kuhofia kuibiwa gari lakini anashukuru Mungu aliiona.

"hii tabia yangu ya kusahau vitu itanitokea puani aisee ona sasa nimeitafuta weee sasa naiona ipo mlangoni na hii siyo mara ya kwanza kwa hili kutokea" Alisema Dude. 

Na Komedi zone



No comments:

Post a Comment