Msanii wa
Komedi Bongo, Hamisi Kihangare ‘Mtanga’ amefunguka kuwa anahofu kumweka
hadharani mkewe hasa kwenye mitandao kwa kuwa anaogopa kuibiwa na kusumbuliwa
na wanaume wakware.
Akipiga
stori na paparazi wetu wa Komedi Zone, Mtanga alisema kuwa ataishia kuwaweka mtandaoni watoto
wake Nadya na Shadya, lakini si kwa mama yao ambaye aligoma kumtaja jina lake
wala kuonesha picha yake kwa kuhofia kuwarahisishia watu kumpata.
“Wewe tambua
tu kwamba mke wangu anaitwa Mama Shadya, jina lake halisi na picha yake sitoa
si unajue naogopa watu nitawarahisishia kumsumbua kirahisi jambo ambalo naogopa
sana,” alisema Mtanga.
Na Komedi zone.

No comments:
Post a Comment