Social Icons

Pages

Tuesday, May 19, 2015

MSANII RINGO AFUNGUKA: 'JAMANI CD ZA BUKUBUKU ZA MTAANI ZINADIDIMIZA UCHUMI WAO NA TAIFA KWA UJUMLA'

Mchekeshaji maarufu kutoka bongo jacob  Mkweche a.k.a. Ringo amefungukia kuhusu  kuendelea kuuzwa  cd za bukubuku  kuwa kunadidimiza uchumi wao na kwa Taifa kwa ujumla.

 Akizungumza na Komedi Zone  Ringo amesema licha ya kuwa kuonesha vipaji vyao kwa mashabiki lakini hali ya kimaisha waliokuwa nayo haifanani na majina walikuwa nayo.
 
Aidha pia amefafanua kuwa baadhi ya wasambazaji wa filamu wamekuwa  hawathamini kazi yao hata kidogo kwa kuwanyonya kwa kuuza filamu zao kwa bei chee kitu ambacho kinawaporomosha kimaisha.
 "Ninaiomba serikali kuingilia katika swala hili vinginevyo mafanikio tutasikia kwenye bomba,"  alisema Ringo

Na Komedi Zone

No comments:

Post a Comment