Social Icons

Pages

Wednesday, May 20, 2015

MTU CHUMA ALIA NA WADAU KUDHARAU WACHEKESHAJI

 Mtu Chuma
MSANII wa komedi ambaye ameonesha kipaji cha hali ya juu katika muvi kama; Mapoda, Noma The Panyaroad na Mbwa Mwitu, Khatibu Mohamedi Mlegelo maarufu kwa jina la Mtu Chuma, amelalamikia kushushwa hadhi kwa wasanii wa komedi nchini.

Akipiga stori na Komedi Zone mapema leo hii, Mtu Chuma alisema kuwa tasnia ya komedi inadharauliwa sana na wadau mbalimbali wa filamu hasa wasambazaji wakubwa wa filamu, jambo ambalo linapelekea kuporomoka kwa mauzo ya kazi zao ambazo mwenyewe alidai kuwa zinapendwa na watu wengi sana kuliko muvi za kawaida.

Mtu Chuma aliongeza kuwa mbali na wasanii wa komedi kutopewa heshima wanayostahili miongoni mwa wadau mbalimbali lakini anashangazwa na jinsi kazi zao zinavyopokelewa kwa wingi na mashabiki zao, jambo linalowafanya wajue wanathamani kubwa lakini wamekosa sapoti.

"Sisi tunajulikana sana kaka lakini tunadharauliwa na wadau, hatupati sapoti hata kidogo jambo linalotufanya tushuke kimauzo. Binafsi nawapongeza sana Komedi Zone kwa kuanzisha blog yetu ambayo itatufanya tusikike," alisema Mtu Chuma.

Na Komedi Zone

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 

No comments:

Post a Comment