Social Icons

Pages

Wednesday, May 20, 2015

SMARTPHONE YAMTOA JASHO MBOTO



MSANII wa komedi mwenye msitu wa vituko, Mboto, amejikuta akitolewa jasho na simu yake ya kisasa 'smart phone' baada ya kuzima ghafla na kupoteza majina ya watu wake wa karibu.

Kwa mujibu wa msanii huyo alisema kuwa simu yake ilianza tatizo hilo siku mbili zilizopita jambo lililomfanya akose mawasiliano na marafiki zake muhimu hadi kufikia hatua ya kuhaha akimtafuta fundi wa kumrekebishia simu yake hiyo.

"Yah si unajua tena hizi simu zetu za smartphone zina mambo mengi, sasa nikashangaa juzi naona laini yangu moja haifanyi kazi na majina hayapo, sasa hivi watu wakinipigia nawauliza majina yao kwanza, hapa namtafuta fundi anirekebishie," alisema Mboto.

Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399 

No comments:

Post a Comment