Ikiwa una Taarifa yoyote kuhusiana na Komedi, tangazo, Filamu mpya na mengineyo tuma kupitia Whatsapp namba +255653146563 au +255765056399
Wakiwa pamoja na Muongozaji wa kipindi hicho Johackim Kapembe kutoka TBC 1
Wakiwa pamoja na muongozaji msaidizi wa Kipindi
Wasanii wa Komedi Bongo zao
la Kaole Sanaa Group, Ujio na Matumaini, wamepata shavu la kurusha maigizo yao
kupitia televisheni ya Taifa ‘TBC 1’ hiyo ikiwa ni moja ya malengo ya wasanii
hao kufanya kazi zenye tija kwa mwaka huu.
Wakipiga stori na paparazzi
wetu, Ujio na Matumaini walisema kuwa huu ni muda sahihi wa wao kujitegemea
zaidi na kuwashukuru wasanii wenzao waliofanya nao kazi kwa karibu enzi za
Kaole kuanzia Ray Kigosi, Marehemu Kanumba, Kipemba, Chiki Mchoma, Cheni, Tito,
Branko , Kissa na wengine wengi.
Naye muandaaji wa kipindi
hicho, Johakim Kapembe wa TBC alisema kuwa ameamua kuwatumia wasanii hao kwa
kuwa wanavipaji vikubwa vya komedi na mashabiki wengi.